0
as_tevez1
Klabu ya West Ham United inafuatilia kwa kina hali ya mambo ilivyo ndani ya klabu ya Juventus kufuatia taarifa kuwa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo ya West Ham Carlos Tevez kugoma kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Juventus.

Kwa mujibu wa gazeti la The Mail on Sunday la nchini Uingereza limeandika kuwa Tevez amegoma kusaini mkataba mpya na vibibi vizee hivyo vya kutoka jijini Turin hivyo wao kwa sasa wanajipanga kumrejesha mshambuliaji huyo kwenye dimba la Boleyn Ground ambapo ilipataja kama ni nyumbani kwa zamani kwa mshambuliaji huyo kwani tayari yeye na Muarjentina mwenzake Javier Marschelano walishapita kwenye klabu hiyo kabla ya kutimkia Manchester United na Liverpool.

 "Itakua ni heshima kubwa sana," Alisema mmiliki wa klabu hiyo alikiambia kituo cha televisheni cha West Ham TV. "West Ham inahitaji kila kilicho bora kwa sasa, na Carito ni mmoja kati ya wachezaji bora sana Duniani wanaowaniwa na vilabu bora na vyenye historia kubwa kama ilivyo West Ham United".

Post a Comment

 
Top