Bao la kipindi cha kwanza
lililofungwa na mchezaji Lazar Markovic lilitosha kuipa ushindi
Liverpool dhidi ya wenyeji wao Sunderland katika uwanja wa stadium of
light.
Licha ya Sunderland kujaribu kufanya mashambulizi katika
lango la Liverpool,ni wageni wao ndio waliodhibiti asilimia kubwa ya
mechi hiyo huku mchezaji Coutinho akiimarisha safu ya kati na ile ya
mashambulizi ya Liverpool.
Liverpool walinyimwa penalty ya wazi
katika dakika za kwanza kabla ya Markovic kuwapita walinzi wa Sunderland
na kucheka na wavu.
Post a Comment