Mshambuliaji nyota wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo,
ametawazwa mshindi wa taji la mchezaji bora duniani, Ballon d’Or, kwa
mara ya tatu kwenye dhifa ya kufana katika makao makuu ya shirikisho la
kandanda duniani, Fifa, Jumatatu jijini Zurich.
Gwiji huyo, 29, aliyeongoza Real Madrid kutwaa taji la kumi la Ligi
ya Mabingwa wa Ulaya, alishinda asimu wake wa jadi na mshindi mara nne,
Lionel Messi wa Barcelona na Argentina, na golikipa wa Ujerumani na
Bayern Munich, Manuel Neuer aliyeshinda Kombe la Dunia kunyakua utukufu
huo.
Ronaldo alikuwa nyota wa sherehe hizo ambazo zilishuhudia mwenzake
wa Real, James Rodriguez, akituzwa taji la bao bora zaidi la mwaka na
kocha wa kikosi cha taifa cha mpira wa miguu cha wanaume wa Ujerumani,
Joachim Leow, akiibuka mshindi wa mwalimu wa mwaka.
“Sikuwahi kufikiria nitashinda kombe hili mara tatu,” Ronaldo
alisema kufuatia kutawazwa kwake akiendelea hamu yake ya kulinyakua tena
haija ishia hapo.
“Natamani kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani wa enzi zote na
hilo linahitaji bidii maridhawa,” Ronaldo aliyeshinda utukufu huo mwaka
jana na 2008 aliendelea.
Straika huyo nyota aliongoza Real kushinda taji la historia la 10
kwa kufuta rekodi ya Messi ya mabao 15 kwenye Ligi ya Mabingwa ndani ya
musimu mmoja kwa kuzaba magoli 17 katika mechi 11.
Orodha ya washindi wa 2014
Ballon d'Or: Cristiano Ronaldo (POR/Real Madrid)
Mchezaji wa wanadada wa mwaka: Nadine Kessler (GER/Wolfsburg)
Kocha wa wanaumme wa mwaka: Joachim Loew (GER/Allemagne)
Kocha wa wanadada wa mwaka: Ralf Kellermann (GER/Wolfsburg)
Taji la Puskas la bao bora zaidi: James Rodriguez (COL/Real Madrid)
Wachezaji wa haki: Wahisani wa kujitolea katika Kombe la Dunia la Brazil 2014
Zawadi ya rais: Hiroshi Kagawa (JPN), mwanahabari wa kandanda
mkongwe zaidi (89) katika dimba la 2014 la Kombe la Dunia ambalo ni la
kumi kuhudhuria kama mwandishi.
Kikosi cha mwaka
Manuel Neuer (GER/Bayern Munich); Sergio Ramos (ESP/Real Madrid),
Thiago Silva (BRA/Paris SG), David Luiz (BRA/Paris SG), Philipp Lahm
(GER/Bayern Munich); Andrés Iniesta (ESP/Barcelona), Toni Kroos
(GER/Real Madrid), Ángel Di Maria (ARG/Manchester United); Arjen Robben
(NED/Bayern Munich), Lionel Messi (ARG/Barcelona), Cristiano Ronaldo
(POR/Real Madrid)
Post a Comment