0
Wenger hits back at Podolski accusations
Meneja wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amezipinga tuhuma alizotuhumiwa na mshambuliaji aliyejiunga kwa mkopo kwenye klabu ya Inter Milan, Lukas Podolski kwamba hakumfanyia heshima alipokuwa anakamilisha uhamisho wake wa mkopo wa kujiunga na klabu hiyo ya Inter Milan.

Podolski – aliyekamilisha uhamisho wa mkopo wa miezi sita wa kujiunga na klabu hiyo ya Inter wiki iliyopita alimtuhumu meneja wake huyo kuwa hakuonesha nidhamu wakati wa kuondoka klabuni hapo kwani hata kumuaga hakumuaga wakati anakamilisha uhamisho huo. 

‘Hajaniambia kitu chochote, hata kunitakia kila la heri pia hajanitakia hajanipigia simu wala kuniaga,’ Podolski aliliambia gazeti la The Sun.

‘sikuhitaji maua wala busu kutoka kwake. Ni heshima tu kuniaga kwakuwa heshima ni kitu kikubwa sana kwetu kama wanaadamu.'

‘Nilifanya kila kitu nilichoweza kuing'arisha klabu yetu kwa uwezo wangu wote. Siamini kama kuna baya au kosa nililotenda wakati nikiwa pale pengine ana tatizo jingine na mimi.'

Wenger, haraka sana amechukua muda wake na kumpatia majibu mshambuliaji huyo kwa kusisitiza kuwa alizungumza na mshambuliaji huyo kabla hajaondoka na kumalizia kwa kusema kuwa bila ya yeye kuidhinisha basi hakuna ambalo lingeweza kutekelezeka.

Post a Comment

 
Top