0
as_sneijder
Meneja wa klabu ya Juventus ya nchini Italia  Massimiliano Allegri ameshindwa kuzificha hisia zake na kutangaza hadharani nia ya kutaka kumjumuisha kikosini mwake kiungo wa klabu ya Galatasaray ya nchini Uholanzi  Wesley Sneijder.

Kwa mujibu wa gaazeti la Tuttosport la nchini Italia limedai kuwa tayari klabu ya Juve imekwishafanya mawasiliano na mchezaji binafsi na ameonesha kuwa na nia ya kutaka kujiunga na kibibbi kizee huyo wa mjini Turin kwenye majira haya ya baridi.

Alipoulizwa kuhusiana na usajili wa mchezaji huyo meneja huyo wa klabu ya Juventus Massimiliano Allegri alisema kuwa Wesley ni aina ya mchezaji ambayo kalabu yake inamkosa kwa sasa hivyo endapo dili hilo litakamilika basi anadhani kuwa Juve itakua imempata mtu mujarabu kabisa ili kutimiza ndoto zao.

Post a Comment

 
Top