Kikosi cha Taifa Stars Maboresho
kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayofanyika
Januari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mechi
hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo kwa
ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza
Ligi za Ndani (CHAN).
Mechi za mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu.
Kocha
Nooij anatarajia wakati wowote kutangaza kikosi cha timu hiyo
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kitakusanyika
Januari 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na siku moja baadaye kwenda
jijini Mwanza.
Post a Comment