0
De Gea future questioned as Valdes nears Man United move
Mashabiki wa klabu ya Manchester United wameachwa midomo wazi juu ya mustakabli wa mlinda mlango wao nmba moja David De Gea mara baada ya hii leo klabu hiyo kutangaza kuwa imefikia makubaliano ya kumpatia mkataba wa miaka miwili mlinda mlango wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Victor Valdes.

Nyanda huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona alishindwa kupata timu ya kuitumikia mara baada ya kuisha kwa mkataba wake kutokana na kuwa majeruhi na hivyo mabosi wa Camp Nou kuamua kuachana naye moja kwa moja.

Licha ya kuhishwa na klabu ya Liverpool, Valdes anatarajiwa kusaini mkataba huo mpya utakao muweka Old Trafford kwa miaka miwili na tayari amekwisha fanya mazoezi na kikosi cha meneja Louis van Gaal kwa takribani miezi miwil. 


Post a Comment

 
Top