Mshambuliaji wa klabu ya Swansea City raia wa Ivory Coast Wilfried Bony amewapasha mabosi wa klabi yake hiyo ya sasa kuwa anataka kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka huu na hivyo ikiwezekana wakubaliane na matakwa yake ya kuuzwa kwenye dirisha hili la usajili la mwezi January.
Ikumbukwe kuwa klabu ya Manchester City tayari imekwishatuma mawakala wake kuulizia thamani ya mshambuliaji huyo mwenye misuli wakati Real Madrid na wao wameshindwa kuzificha hisia zao juu ya hitaji lao la kutaka kumsajili mshambuliaji huyo.
Post a Comment