Klabu ya Manchester United iko katika hatua za mwisho mwisho kabisa kukamilisha dili la mlinzi wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund Mats Hummels ambapo imethibitishwa kuwa United imekwishatuma ofa babukubwa kwa klabu ya Borussia Dortmund kuishawishi kumuuza mchezaji huyo.
Hummels ameibuka kuwa mmoja ya wachezaji wanaowindwa kwa udi na uvumba na klabu ya Manchester United kwa miezi ya hivi karibuni huku meneja Louis van Gaal akiwa katika harakati za kumsajili mlinzi wa kiwango cha Dunia kuimarisha sehemu yake ya ulinzi wa klabu hiyo.
Dortmund tayari wamekwishatangaza kuwa mchezaji huyo hauzwi kwenda klabu yoyote ile lakini mwandishi mmoja raia wa Italia Gianluigi Longari ameandika kuwa tayari klabu ya Manchester United imekwishatuma ofa kabambe kwa klabu hiyo.
Haijatajwa hadharani ni kiasi gani cha pesa kilichotumwa na klabu ya ya Manchester United katika kuhakikisha kuwa dili la Hummels lakini inakisiwa kuwa ni takribani paundi milioni 30.
Post a Comment