KLABU ya Yanga imetuma CAF majina ya wachezaji 23 watakaoshiriki
katika michuano ya kombe la shirikisho Afrika huku jina la mkongwe kipa
Juma Kaseja likikosekana.
Kaseja aliyekosa namba kwenye kikosi cha Yanga tangu alipojiunga nayo
kwenye dirisha dogo msimu uliopita hajahudhuria kwenye mazoezi ya timu
hiyo tangu ilipoanza maandalizi ya mechi za raundi ya nane kwa sababu ya
kutocheza kwenye kikosi cha kwanza.
Afisa mawasiliano wa klabu ya Yanga Jery Muro, amewaambia waandishi wa habari
kuwa wameliondoa jina la Kaseja kwasababu ameshindwa kufanya mazoezi na
wenzake kwa kipindi cha mwezi mmoja bila sababu maalumu huku akiendelea
kulipwa mshahara kama kawaida.
Yanga imepangwa kuanza na klabu ya BDF kutoka Botswana ambayo ni timu inayomilikiwa na jeshi la ulinzi la nchi hiyo.
Post a Comment