0
Mwalimu wa timu ya taifa ya Rwanda, Stephen Constantine amejiuzuru kuwa kocha watimuhiyo amethibitisha msemaji wa chama cha soka cha Rwanda Football Federation (Ferwafa), Moussa Hakizimana.

Kwa mujibu wa Hakizimana, Constantine ametuma barua hiyo ya kujiuzuru kwa Ferwafa kupitia barua pepe (email) siku ya jana akithibitisha kuwa hataendelea kuwa kocha wa Amavubi.

Kwenye taarifa yake, Hakizimana alisema, “Stephen Constantine hatakua tena kocha wa timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi ) kwani amepata kazi nchini India ambayo ina mshahara na malipo mazuri kuliko tunayompatia sisi.”

Imefahamika kuwa Muingereza huyo alikua akilipwa kiasi cha dola 11,000 za kimarekani kwa mwezi na tangu aanze kazi ya kukinoa kikosi hicho angalau amefanikiwa kukipandisha kikosi hicho kwenye viwango vyq FIFA vya usakataji kabumbu duniani akiitoa timu hiyo kutoka nafasi ya 134 mpaka ya 68 inayoishikilia kwa sasa.


Post a Comment

 
Top