Mzozo kati ya Lionel Messi na kocha Luis Enrique na kutimuliwa kwa
mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta baada ya marufuku ya kutonunua
wachezaji kudumishwa, vimesababisha mgogoro mkubwa katika bodi ya klabu
ya Barcelona.
Kashfa huwa sana hazijitengi na klabu hiyo ya Catalona ambayo
imekumbwa na mizozo si haba, hasa kutokana na umuhimu wa klabu hiyo kwa
jamii.
Lakini hakujakuwepo na mtafaruku mkubwa sawa na wa sasa tangu siku za
rais Joan Gaspart, ambaye usimamizi wake mbaya ulipelekea yeye
kujiuzulu na uchaguzi kufanywa 2003.
Chini ya mwaka mmoja uliopita, rais wa wakati huo Sandro Rosell
alijiuzulu baada ya jaji kuamua kuchunguza ununuzi wa Neymar kutoka
Santos baada ya kesi hiyo kuwasilishwa na shabiki.
Nafasi yake ilichukuliwa na makamu wa rais Josep Maria Bartomeu,
ambaye mara moja alikiri bei aliyonunuliwa nyota huyo wa Brazil ilikuwa
karibu na €100 milioni badala ya €57.1 milioni zilizoripotiwa awali.
Kumekuwepo na miito ya kufanyika kwa uchaguzi wa urais, lakini
Bartomeu amezidi kusisitiza kwamba atakamilisha muhula wake na bodi,
ambao unamalizika 2016.
Umekuwa mwaka wa masaibu kwa Bartomeu, ambao sasa unafika kileleni
kufuatia kuondoka kwa Zubizarreta na kushindwa kwa timu hiyo kuridhisha
chini ya Luis Enrique.
Mashabiki walieleza wazi msimamo wao video ilipochezwa uwanjani Nou
Camp kusherehekea Messi kuvunja rekodi ya ufungaji mabao La Liga Novemba
iliyopita na video ya Bartomeu na Zubizarreta ikaibua kelele.
Rekodi ya Zubizarreta sokoni kipindi alichohudumu kama mkurugenzi wa
michezo tangu 2010, urais wa Rosell ulipoanza, ni mbaya mno.
Tangu mwanzo, hakuwa na ushirikiano wa karibu na kocha
Pep Guardiola ambao mtangulizi wake Txiki Begiristain, aliye sasa Manchester City, alijuvunia.
Pamoja na kashfa ya Neymar, Zubizaretta mwaka uliopita alilaumiwa kwa
kutoimarisha safu ya ulinzi, ambayo ilikuwa imelala msimu uliopita
klabu hiyo iliposhindwa kushinda taji lolote kubwa.
Alipotumia pesa kabla ya msimu kuanza, mashabiki walitamaushwa na
kununuliwa kwa mzee Jeremy Mathieu kutoka Valencia na jogoo la shambani,
Mbrazil Douglas.
Marufuku ya Fifa ya kutonunua wachezaji vipindi viwili kwa kukiuka
kanuni za ununuzi wa wachezaji wa kigeni wasiotimiza umri wa miaka 18
ndiyo iliyoharibu mambo kabisa.
Kiti cha Zubizarreta kiliwaka zaidi alipoambia runinga ya Uhispania
Jumapili usiku kwamba rais wa klabu hiyo pia anawajibikia marufuku hiyo.
"Bartomeu alikuwa wakati huo makamu wa rais aliyehusika na michezo na
alifahamu vyema hali ilivyokuwa,” Zubizarreta aliambia Canal Plus.
Hilo lilipelekea Barcelona kumfuta Zubizarreta siku iliyofuata, huku
mkutano wa dharura wa bodi ukipangiwa Jumatano kujadili mrithi wake.
Hali kwenye bodi ingekuwa rahisi iwapo hawangekuwa pia wakitatizwa na
presha kuhusu Luis Enrique baada yao kulazwa ugenini na Real Sociedad
Jumapili, na jumla ya matokeo mabaya.
Kocha huyo alishangaza kwa kuwaacha Messi na Neymar kwenye benchi kwa
mechi hiyo, na tabia yake ya kubadilisha badilisha wachezaji pia
imepelekea wengi kumkashifu kwa kukosa mwelekeo.
Lile linaloweza kuamua mustakabali wake ni uhusiano wake na Messia ambao unaonekana kusambaratika.
Nyota huyo wa Argentina alijibizana na kocha huyo mazoezini Ijumaa
iliyopita na kisha Jumatatu akakosa kuhudhuria kikao wazi cha mazoezi na
ziara ya sikukuu hospitalini kutembelea watoto wagonjwa, huku klabu
hiyo ikisema alikuwa anaugua.
Luis Enrique ni kigogo lakini inaonekana huenda aambulie patupu
kwenye vita vyake na mchezaji huyo aliyeshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa
Mwaka Duniani mara nne.
Chanzo:- Supersport.com
Post a Comment