Ronaldo, Balotelli au Hamsik? Huu ni wakati wako sasa kwa mwanamichezo kumchagua mcheza soka ambaye alikua na unyoaji uliokuvutia sana kwa mwaka 2014. Mtandao wa Goal.com umekuletea shindano jipya linalowashindanisha wachezaji mahala pote Duniani kuwania nafasi ya kuwa mtu aliyenyoa unyoaji wa kuvutia zaidi ambapo msomaji atatakiwa kumpigia kura mtu anayedhani alikuwa na aina ya unyoaji wa ajabu au wa kuvutia.
Mwanzishaji wa mashindano haya bwana Daniel Johson amewateuwa wachezaji takribani 20 wakiwa na aina za unyoaji tofautitofauti hivyo kuwapa nafasi wafuatiliaji wa masuala ya soka kumchagua wanayedhani aliwazidi wachezaji wengine kwa kuwapigia kura kupitia mtandao wa Goal.com na mshindi wake anatarajiwa kutangazwa Januari 8.
Orodha kamili ya wachezaji wanaowania tunzo hiyo ni kama inavyoonesha hapo chini.
- Alexis Sanchez
- Andrea Pirlo
-
Arturo Vidal
-
Bacary Sagna
-
Brek Shea
- Dani Alves
- Cristiano RonaldoDeAndre Yedlin
-
Dominic Oduro
-
James Rodriguez
-
Kyle Beckerman
- Marek Hamsik
-
Marouane Fellaini
-
Mario Balotelli
-
Neymar
- Nicklas Bendtner
-
Paul Pogba
-
Rodrigo Palacio
-
Stephan El Shaarawy
- Ze Roberto
Post a Comment