0
Blanc bans Lavezzi and Cavani for two gamesKocha wa klabu ya PSG,Laurent Blanc amewafungia michezo miwili washambuliaji Edinson Cavani na Ezequiel Lavezzi kuitumikia timu hiyo ya Paris Saint-Germain mara baada ya kuchelewa kwa takribani siku nne wakitokea kwenyemichuano ya kimataifa. 

Wachezaji hao hawakuandamana na kikosi cha timu hiyo kilicho kilichokwenda kujiandaa kwaajili ya michuano mbalimbali kwenye kambi ya nchini Morocco mara baada ya kuamua kuchelewa ili wapate muda wa kukaa na familia zao.

Ikumbukwe kuwa wawili hao, Cavani na Lavezzi wamekua wakihusishwa na kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo inayotarajiwa kumenyana na klabu ya Montpellier kwenye michuano ya Coupe de France mnamo siku ya kesho jumaatatu.

 PSG imewaamuru wawili hao kufanya mazoezi kando na wenzao na ukiachilia mbali mchezo dhidi ya Montpellier lakini pia watakua watazamaji kwenye dimba la Stade de la Mosson na tripu ya siku ya jumaapili kwenda kupambana na Bastia kwaajili ya mchezo wa Fench League 1. 


Post a Comment

 
Top