Inter Milan wamesaini kiungo nyota cha Usiwi, Xherdan Shaqiri kutoka
magwiji wa Ujerumani, Bayern Munich, kwa mkopo wa miezi sita, klabu
hicho cha Serie A kimetangaza Alhamisi.
Inaripotiwa Inter wamekubali kulipa euro milioni mbili kusajili
kiungo hicho cha pembeni na chaguo la kumnunua kwa kitita cha euro
milioni 14 ifikapo Juni katika mkataba wa kudumu.
“Makubaliano yamekamilika kati ya Inter Milan na Bayern Munich
katika kuwasili kwake (Xherdan Shaqiri) nerazzurri,
sahihi ndio inakosa pekee,” mabingwa hao wa zamani wa Ulaya waliandika
kwenye anwani yao rasmi ya mtandao wa kijamii wa Twitter.
Shaqiri ambaye alihitimu kutoka chuo cha chipukizi cha Basel
alifungia Uswisi mabao matatu kwenye Kombe la Dunia lakini amekaushwa
nafasi Bayern na mwalimu Pep Guardiola kwani anashindania kuanza na
magwiji Arjen Robben na Franck Ribery pembeni.
Anafuata nyayo za nyota wa Kombe la Dunia wa Ujerumani na mshambuliaji Lukas Podolski kuwasili Inter Milan.
Post a Comment