Vilabu
vya Yanga, Azam na KCCA jana vimekumbana na vipigo katika mechi za Robo
Fainali ya Kombe la Mapinduzi na kutupwa nje ya michuano hiyo.
Azam wamepokea kipigo kutoka kwa Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida.
Nayo KCCA ya Uganda imetolewa na Polisi Zanzibar kwa mikwaju ya Penati baada ya sare katika muda wa kawaida.
Kwa upande wa Yanga katika mchezo uliomalizika majira ya saa 4.30 Usiku,
imepigwa mshangao baada ya kuchapwa bao 1-0 na JKU ya Zanzibar.
Simba tayari ilikwisha tangulia kwa kupata ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Taifa Jang'ombe jana.
Kwa matokeo haya, Nusu Fainali itakuwa ni kama ifuatavyo;-
Simba Vs Polisi Zanzibar
Mtibwa Vs JKU.
Post a Comment