KATIKA kile kinachoonesha kuchoshwa na utani uliopitiliza wa mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich Thomas Müller, mlinzi raia wa Brazil anayekipiga kwenye klabu hiyo Dante amepeleka malalamiko yake rasmi kwa viongozi wa juu wa klabu hiyo kuhusu mshambuliaji huyo kumtania kuhusiana na kichapo cha timu yake ya taifa cha jumla ya magoli 7-1 dhini ya Wajerumani hao kwenye fainali za kombe la Dunia zilizofanyika nchini Brazil.
Kwenye malalamiko hayo Dante amesisitiza kuwa tangu warejee kutoka kwenye fainali hizo amekuwa hana raha na mshambuliaji huyo kutokana na kichapo hicho kugeuzwa kuwa fimbo ya kumchapia kwa kila anachokifanya klabuni hapo.
Dante alikwenda mbali zaidi kwa kupiga mkwara mzito kuwa endapo mshambuliaji huyo ataendelea kumtania utani huo kitakachofuata baina ya wawili hao ni kuchapana makonde mpaka mbabe ajulikane kwani utani huo kwa ukweli unamnyima raha ya kufaya kazi klabuni hapo.
Post a Comment