Makabiliano kati ya Arsenal na Stoke City Jumapili ugani mwao
Emirates Jumapili yanapatia mwalimu Arsene Wenger nafasi ya kufuta
machungu ya kulazwa na wapinzani hao kwenye matokeo yaliomtatiza pakubwa
katika utawala wake mrefu wa miamba hao.
Wenger amestahimili shutuma kali kutoka mashabiki wa Arsenal misumu
ya hivi karibuni lakini vilio dhidi yake vilifika kiwango kipya cha
laana baada ya timu yake kushindwa 3-2 ugenini Britannia Stadium mwezi
uliopita.
Mwalimu huyo alitupiwa cheche za matusi na mashabiki waliojawa na
hamaki alipokuwa anaabiri gari la moshi katika kituo cha Stoke na licha
ya matokeo kuimarika katika mechi zilizofuata, kukomeshwa 2-0 na
Southampton katika mechi iliyopita kulizua malalamishi tena kutoka
wafuasi wa klabu hicho.
Wengi wametaka aondolewa mamlakani na hakuna lingine ila ushindi
dhidi ya vijana wa Mark Hughes kutasitisha kelele zinazolenga kumaliza
utawala wa Wenger uliogonga miaka 17 mwaka jana.
Arsenal wanaketi nafasi ya sita, alama tatu nje ya nafasi za nne
bora za kufuzu Ligi ya Mabingwa na wana jukumu la kufuatanisha mkimbio
wa matokeo bora ili kuhifadhi mazoea yao kama vizingiti mwa nafasi hizo
bora.
Wenger anakwamilia kuwa dua linabadilikia kikosi chake baada ya kukumbwa na majeraha mengi katika muhula wa kwanza wa musimu.
Mabeki Laurent Koscielny na Mathieu Debuchy wamerudia hali sawa ya
kucheza na viungo Aaron Ramsey, Mesut Ozil na Mathieu Flamini walirudi
wote mazoezini juma hili.
“Tunazidi kupata nguvu sasa. Tunaweza faidikia kutoka hilo
kwasababu hawa ni wachezaji ambao hawajashoshwa na mechi mingi. Wanarudi
na watatupatia udhibiti miezi ijayo,” Wenger alisema.
Mwalimu huyo atakaribisha tena mshambuliaji nyota Olivier Giroud
ambaye ametumikia marufuku ya mechi tatu baada ya kupata kadi nyekundu
kwa uhasama uwanjani katika mechi yao dhidi ya QPR Desemba 26.
Chanzo: Supersport.com
Post a Comment