Mechi za kwanza za raundi ya pili ya
mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake-Tanzania (Taifa Cup
Wanawake) zinachezwa wikiendi hii (Januari 17 mwaka huu) kwenye miji
minane tofauti nchini.
Timu tisa zilizofuzu kutoka raundi ya
kwanza baada ya mechi za nyumbani na ugenini akiwemo mshindwa (best
loser) zitaungana na Ilala, Kinondoni na Temeke kucheza raundi ya pili.
Mechi za marudiano za raundi hiyo zitachezwa Januari 21 mwaka huu.
Hatua
ya robo fainali itakayochezwa Januari 26 na 27 mwaka huu pamoja na nusu
fainali na fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Proin Promotions
itafanyikia jijini Dar es Salaam.
Post a Comment