Southampton walifikisha kikomo mkimbio wa Manchester United wa
kutoshindwa mechi 10 na kuwapita kuingia nambari tatu Ligi ya Premia
baada ya kuwacharaza 1-0 uwanjani Old Trafford Jumapili.
Baada ya kipindi cha kwanza cha vuta nikuvute ambapo pande zote
mbili zilishindwa kulenga wavu, nguvu mpya wa Southampton Dusan Tadic
alifunga bao la ushindi dakika ya 69 na kuwapa United kichapo na
kupunguza matumaini ambayo yalikuwa yamerejea Old Trafford.
Southampton, walionyamazisha United kwa uchezaji stadi ugenini, wana
alama 39 kutoka kwa mechi 21, huku United sasa wakishuka hadi nambari
nne na alama 37.
Awali, Alexis Sanchez alifunga mabao mawili na kusaidia ufungaji wa
la tatu na kuwezesha Arsenal kulaza Stoke City 3-0 uwanjani Emirates na
kupita Tottenham Hotspur na kuingia nambari tano wakiwa na alama 36.
Post a Comment