Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ametwaa tuzo nyingine katika kipindi cha siku tatu zilizopita baada ya kutajwa kuwa mchezaji bora wa muda wote kwenye historia ya soka la Ureno .
Ronaldo
ametwaa tuzo hiyo katika hafla maalum iliyoandaliwa kwenye Gala Quinas
De Ouro iliyofanyika huko Ureno ikiwa imeandaliwa kutoa tuzo za heshima
kwa wanasoka mbalimbali wa Ureno ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka
100 ya shirikisho la soka la ureno.
Ronaldo
ametwaa tuzo hiyo akiwa amepigiwa kura nyingi kuliko magwiji wa soka wa
Ureno akiwemo Luis Figo na hayati Euesebio ambaye alifariki dunia mwaka
jana baada ya kuugua maradhi ya kiharusi kwa muda mrefu
Ronaldo
ametwaa tuzo hiyo baada ya mafanikio aliyoyapata hasa akiwa na klabu
ambapo ametwaa mataji karibu yote akiwa na Manchester United na Real
Madrid .
Zaidi
ya hapo Ronaldo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara
tatu akiwa mreno pekee kutwaa tuzo hiyo mara tatu hali ambayo imechangia
kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa Ureno kwa miaka yote.
Hafla
ya utoaji tuzo hizo ilihudhuriwa na marais wa FIFA na UEFA Sepp Blatter
na Michel Platinni na Ronaldo hakuweza kuhudhuria tuzo hiyo na
ilichukuliwa kwa niaba yake na wakala wake Jorge Mendez.
Post a Comment