Arsene Wenger amethibitisha kuwa yuko njiani kuwapiga bei au kuwatoa kwa mkopo washambuliaji wawili wa klabu hiyo kwenye dirisha hili la usajili la mwezi January.
Lukas Podolski tayari amekwishajiunga kwa mkopo wa muda mrefu kwenye klabu ya Inter Milan na sasa Wenger anataka kumtoa mshambuliaji kinda Yaya Sanogo katika kutimiza adhima hiyo.
Mfaransa Sanogo ameonekana kuivutia klabu ya Bordeaux kwa makubaliano ya kumnunua moja kwa moja lakini Wenger anaonekana kutokuwa tayari kumuuza moja kwa moja isipokuwa kumtoa kwa mkopo.
‘Kwa sasa Yaya Sanogo yuko Arsenal Yuko tofauti sana sana na[Lukas]
Podolski – Podolski alikua amekata tamaa lakini Sanogo anatafuta uzoefu ili ajiimarishe zaidi,’
Alisema Wenger alipohojiwa na waandishi wa habari mara baada ya ushindi wa juml ya magoli 2-0 wa michuano ya FA Cup dhidi ya Hull City.
‘Kwa upande wangu, Nimekwisha sema mara kadhaa kuwa natamani sana kumuona bwana mdogo akiendelea kubakia na kucheza kwenye Premier League ili aweze kupata uzoefu zaidi.’
Joel Campbell naye ni mshambuliaji mwingine anayetajwa sana kuwa huenda akatolewa kwa mkopo au kuuzwa msimu huu.
Post a Comment