0
Stephen Constantine is carried by his Rwandan players after victory over Congo Brazzaville in Kigali

Kocha mkuu wa  timu ya taifa ya Rwanda Stephen Constantine ametaja majina ya wachezaji 25 wa kikosi cha awali cha timu yake watakao pambana na vijana walio chini ya umri wa miaka 23 wa Tanzania watakaojitupa dimbani siku ya tarehe 22 ya mwezi huu jijini Mwanza. 

Mwanzoni mchezo huu ulitakiwa uchezwe siku ya tarehe 9 ya mwezi Desemba mwaka jana ambayo ni siku ya uhuru wa Tanzania lakini Rwanda waliomba mchezo huo kuahirishwa mpaka wakati mwingine kwani wachezaji wake wengi walikua wakijiandaa kwaajili ya mashindano ya Ombudsman Cup yaliyofanyika mnamo Desemba 6-8 nchini Rwanda.

Akizungumza na mtandao wa Supersport.com, mwalimu Constantine alisema, “hii ni nafasi ya pekee kwetu kukipima kikosi chetu cha vijana walio chini ya umri wa miaka 23 ambao wanatarajiwa kucheza mchezo wa kufuzu kwaajili ya michuano ya Olympic mnamo mwezi March. Tanzania inakikosi imara mabacho ninaamini kitakua kipimo muafaka sana kwetu kuelekea mchezo huo.

Constantine amemjumuisha kikosini nahodha wa Amavubi, Haruna Hakidhimana Fadhili Niyonzima, anayekipiga kwenye klabu ya Dar es salaam Young Africans. ambaye ataungana na Ismael Nshutiyamagara (APR), Jean Baptiste Mugiraneza (APR), Ernest Sugira (AS Kigali) na Jean Claude Zagabe (Mukura) kama wachezaji ambao wamezidi umri wa miaka 23 kama sheria ya michuano hiyo ya Olympic inavyotaka kila timu kuwajumuisha wachezaji watatu waliopita umri huo ili kuboresha vikosi. 

Kwa mara ya mwisho Niyonzima alikitumikia kikosi cha timu yake ya taifa kwenye mchezo ambao Mnyigu hao waliibuka na ushindi wa jumla ya magoli 4-3 dhidi ya Congo Brazzaville mnamo mwaka 2015 kwaajili ya kufuzu kwa michuano ya Afrika (Africa Cup of Nations) ambapo Rwanda walitolewa mashindanoni mara baada ya kubainika kumchezesha mchezaji mmoja mwenye utambulisho wa aina mbili tofauti Dady Birori alias na Tady Etekiama Agiti.

Rwanda itapambana na Somalia kwanye mchezo wa awamu ya kwanza kabla ya mshindi wa jumla kuwavaa Uganda na mshindi atapambana na Mafarao wa Misri kwenye mchezo wa kufuzu kwa fainali CAF ambapo fainali zake zitapigwa zitapigwa nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo ambapo washindi watatu wa juu watakua wamefuzu kwaajili ya michuano ya Olympic ya mwaka 2016 jijini Rie de Jenairo nchini Brazil.

Mnamo mwezi November, Rwanda walikua ugenini kukipiga dhidi ya Morocco kwenye mchezo uliopigwa jijini Marrakesh na kumalizika kwa sare ya kutofungana kabla ya kufuatiwa na sare nyingine ya kutokufungana dhidi ya Burundi jijini Bujumbura.

 Kikosi cha awali kinawajumuisha.

Walindamlango: Marcel Nzarora (Police), Olivier Kwizera (APR) and Steven Ntalibi (Police). 

Walinzi: Soter Kayumba (AS Kigali), Ismail Nshutiyamagara (APR), Emery Bayisenge (APR), Michel Rusheshangoga (APR), Fitina Ombelenga (SC Kiyovu), Janvier Mutijima (AS Kigali) and Eric Rutanga (APR).

Viungo: Haruna Niyonzima (Yanga), Jean Baptiste Mugiraneza (APR), Rachid Kalisa (Police), Justin Mico (AS Kigali), Savio Nshuti Dominique (Isonga), Patrick Sibomana (APR), Jean Claude Zagabe (Mukura), Kevin Muhire (Isonga), Andrew Buteera (APR) and Emmanuel Sebanani (Police). 

Washambuliaji: Ernest Sugira (AS Kigali), Danny Usengimana (Isonga), Bertrand Iradukunda (APR), Innocent Ndizeye (Amagaju) and Issa Bigirimana (APR).

Post a Comment

 
Top