Meneja wa klabu ya PSG Laurent Blanc ameshindwa kuzificha hisia zake na ametangaza nia ya kutaka kufanya kazi na mtukutu Mario Balotelli aka Super Mario.
Licha ya utukutu uliooneshwa na mshambuliaji huyo pale Anfield msimu huu, Balotelli bado ana mashabiki wengi sana ulimwenguni na Ufaransa kwenyewe.
Wakala wa Balotelli, Mino Raiola, tayali ameshathibitisha kupokea ofa kutoka kwa mabosi wa klabu ya PSG na yuko kwenye mchakato wa kuwalazimisha Liverpool kumruhusu mchezaji huyo akacheze kwa mkopo kwenye League 1.
PSG inatarajia kumuachia Edinson Cavani, kwenda akutakako endapo tu wakala Raiola atafanikiwa kuwashawishi Liverpool kukubaliana na matakwa ya mteja wake na PSG kwa ujumla na inatarajiwa kuwa uamuzi wa kumuachia au kuto kumuachia utategemeana na endapo kama klabu hiyo itampata mbadala wa Balotelli.
Post a Comment