0
Juventus's Swiss defender Stephan Lichtsteiner shows his frustration at the end of the 1-1 draw agai 
Klabu za Inter Milan na Juventus usiku wa jana zilitoka sale ya goli 1:1 kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Italia. Mchezo huu ulikua ukisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa kandanda ulimwenguni kutokana na klabu ya Inter kufanya mabadiliko madogo kwenye klabu hiyo siku za hivi karibuni.

Intermilan walimtimua Walter Mazzari na kumrejesha meneja wake wa zamani Roberto Manchini huku siku chache zilizopita wakimnasa kwa mkopo mshambuliaji raia wa Ujerumani Lucas Poldoski.

Poldoki alianzia benchi kwenye mchezo huo ambao Carlos Tevez aliifungia klabu ya Juve goli la kuongoza mnamo dakika ya tano tu ya mchezo kabla ya Leonardo Bonucci kuisawazishia kwa shuti kali kutoka katikati ya uwanja. 

Poldoski amewaonesha mashabiki wa klabu ya Inter ni kitu gani walikua wanakikosa kwa muda mrefu kutokana na uwezo wake wa hali ya juu wa kusakata kabumbu aliouonesha kwenye mchezo huo haswa likija suala la mashuti ya mbali.

Post a Comment

 
Top