0
Mrwanda katusababishia ukame- Adolf Risharld

KOCHA wa Polisi Moro Oddofu Risharld amesema anamkumbuka sana mshambuliaji mkongwe aliyejiunga na Yanga kwenye dirisha dogo Danny Mrwanda kwa sababu timu yake imekuwa na ukame wa mabao tangu raundi ya nane ilipoanza.

Risharld ameuambia mtandao wa Goal.com  kuwa anaumiza kichwa namna ya kuwatengeneza washambuliaji waliopo ili waweze kufanya kama vile alivyokuwa akifanya Mrwanda na kuipa mafanikio timu hiyo isiweze kushuka daraja.

“Tumecheza mechi mbili bila kufunga hata bao mmoja safu yangu ya ushambuliaji imekuwa butu kibaya zaidi hakuna tena muda wa kusajili na washambuliaji waliopo Said Bahanuzi na Salum Machaku bado wanahitaji muda ili kuweza kuelewana na kufanya vizuri,”anasema Risharld.

Mrwanda amefunga mabao 4 akiwa Polisi Moro kabla haja sajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili mshambuliaji huyo amekuwa na kipaji kikubwa cha kufunga mabao tangu alipokuwa akiichezea klabu ya Long Han Tan An ya Voetnam.

Post a Comment

 
Top