Kocha wa Atletico Madrid Diego
Simeone amesema Fernando Torres amerejea kuwa ''mwanaume'' ndivyo
alivyomuita hivyo baada ya mshambuliaji huyo kufunga magoli yake ya
kwanza tangu alipojiunga na Atletico madrid.
Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Torres alijiunga na Liverpool mwaka 2007.
Torres
alijiunga na Atletico mwanzoni mwa mwezi huu na aliifungia klabu hiyo
magoli mawili katika dimba la Bernabeu na kutoka sare ya mabao 2-2
ilipokutana na Real Madrid katika michuano ya Copa del rey.
Torres naye ameonesha furaha yake na kushukuru wapenzi wake kwa kumuunga mkono.
Post a Comment