Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA
limeahidi kutoa dola laki Saba na nusu kwa shirikisho la soka la
Tanzania kwaajili ya maandalizi ya Timu ya Taifa Tanzania kuelekea kombe
la Dunia mwaka 2018.
Shirikisho la soka la Tanzania (TFF)
limepokea Taarifa kutoka Fifa ya kupatiwa fedha kwa ajili ya Maandalizi
ya Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ( Taifa stars ) ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la Dunia mwaka 2018.
Kwa
upande wake Rais wa shirikisho hilo Jamal malinzi Amethibitisha Taarifa
hiyo kuwa FIFA Imeahidi kuwapatia fedha kwaajili ya kufanya maandalizi
ya Timu ya Taifa kusaka tiketi ya kushiriki kombe la Dunia .
Malinzi
amesema kiasi hicho cha fedha pia watakitumia kuanzisha miradi
mbalimbali ili kuliwezesha shirikisho kuwa na fedha za kutosha na
kuendeleza shughuli za kimichezo kwa upande wa soka.
Post a Comment