0
as_luisenriqueMeneja wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania Luis Enrique amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo kwakuwasihi kuto paniki kwa kItendo cha kutupiliwa mbali rufani yao waliyoikata mahakama ya kimataifa ya masuala ya michezo CAS ya kupinga kufungiwa kufanya usajili kwa miaka miwili.

" Halikua jambo la kushangaza sana pale tulipoarifiwa kuwa rufani yetu imetupiliwa mbali na wenye mpira wao, sisi kama Barca tunatambua vita iliyopo mbele yetu na wao lakini pia sisi kama klabu tumejipanga kwa umakini mno kuhakikisha hatukumbani na mapungufu yoyote mara baada ya kufungiwa kwetu kufanya usajiLi."

" Ukifuatilia kwa umakini utaweza kugundua kuwa klabu imepitia vikwazo mbalimbali katika vipindi tofauti na imefanikiwa kupambana navyo na hatimaye kufikia katika mafanikio iliyonayo sasa hivyo hii sio jambo la ajabu sana kwa klabu yetu".

Enrique alisisitiza kuwa huu ni wakati muafaka kwa wachezaji chipukizi wa klabu hiyo kuonesha uwezo wao na yeye kama mwalimu amekwisha wafungulia milango wachezaji hao ili waweze kuonesha uwezo wao na hatimaye waweze kuwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

"Kuna wachezaji kadhaa wa kikosi B cha klabu yetu ambao nimevutiwa nao vya kutosha, Hii ni sera yetu ya klabu yetu kwani mara zote huwa tunategemea zaidi kikosi B kuliko madirisha mbalimbali ya usajiri, La Masia ndio mwokozi wetu siku zote na tunaamini tutafanikiwa katika hili linalotukabili kwa sasa.

Post a Comment

 
Top