0
“Umakini unahitajika kuchukua Ubingwa”- Hans van der Pluijm

KOCHA wa Yanga, Hans van der Pluijm ameonekana kuifungia kazi safu yake ya ushambuliaji kwa kutaka ifunge mabao mengi katika kila nafasi watakayoipata wanapokuwa kwenye mechi.

Pluijm raia wa Uholanzi ameiambia Goal.com kuwa, hakufuraishwa kuona timu yake ikitolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi na JKU kutokana na kupoteza nafasi nyingi za mabao walizozipata.

“Tunaelekea kwenye ligi pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho Afrika lazima tuwe makini ili tufikie lengo nataka tuchukue ubingwa wa ligi ya Vodacom na tufike angalau hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho,”amesema Pluijm.

Yanga inashika nafasi ya nne kwenye ligi kuu ikiwa na pointi 14 sawa na mabingwa watetezi Azam lakini zinazidiana uwiano wa mabao.

Post a Comment

 
Top