0
Former Manchester United manager David Moyes has been offered the top job at Real SociedadKocha wa Real Sociedad David Moyes alisifu timu yake kwa kujilinda vyema wakati wa ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Barcelona Jumapili. 

Moyes hakupata raha mwaka mmoja uliopita lakini alijaa tabasamu baada ya timu yake kukaa imara na kulaza Barca baada ya kujipata kifua mbele dakika ya pili kupitia bao la kujifunga lake Jordi Alba. 

Raia huyo wa Scotland hakumaliza msimu mmoja akiwa Manchester United kabla ya kufutwa Aprili na alichukua kazi ngumu alipokubali kuwa mkufunzi wa Sociedad wanaopigana vita vya kuzuia kushushwa daraja Novemba. 

 Moyes' reign at Old Trafford lasted just 10 months as the Scotsman failed to get the best out of his players

Kulikuwa na shaka vyombo vya habari kutokana naye kukosa tajriba ya soka ya Uhispania, na kutoweza kwake kuzungumza Kihispania, lakini ameanza vyema, akizidi kuimarika na kufikia sasa wamepoteza mechi moja pekee. 

“Ninafurahia sana kupata matokeo hayo, ilikuwa mechi muhimu sana na mechi ngumu sana,” Moyes aliambia kikao cha wanahabari.

“Tuliweka bidii sana kujilinda na kujilinda ni sehemu kuu sana ya kandanda. Huwezi kushinda mechi iwapo hujilindi vyema. Tulivyocheza nyuma ilitupa nafasi ya kushinda mechi. 

 

"Huwa daima natumai tupate mpira mechi zetu zote lakini dhidi ya Barcelona mnajua hilo ni ngumu. 

“Hilo ni jambo tunaloweza kujiboresha lakini ninataka kusisitiza moyo wa timu na tulivyotia bidii pamoja.” 

Kibarua cha Sociedad kilikuwa rahisi kiasi Lionel Messi na Neymar wakiwa kwenye benchi kipindi cha kwanza na walirudi Ijumaa iliyopita kutoka likizo yao ya Krismasi na Moyes alisema hakushangazwa na timu iliyotumiwa na kocha wa Barca Luis Enrique. 

 

"Siwezi nikasema kwamba ilikuwa rahisi kwani Barcelona wana kikosi kikubwa chenye wachezaji nyota,” akasema. 

“Wana wachezaji nyota hata hivyo lakini hawawezi kuwa sawa mechi zao zote. 

"Mechi muhimu zaidi kwa Barcelona zitakuwa baadaye kwenye msimu na nadhani Luis Enrique alitumia busara. Nilifikiria jambo kama hili lingefanyika na tulijiandaa.”

Chanzo Supersport.com 

Post a Comment

 
Top