Mlinzi wa zamani wa klabu ya Barcelona, Carles Puyol ametangaza kuachana na nafasi yake ya usaidizi wa ukurugenzi wa michezo wa klabu hiyo.
Puyol
ameishikilia nafasi hiyo kwa takribani miezi mitatu na nusu na sasa kwa hiyari yake ameamua kuachana na kazi akiwa kama vile anamfuata mkuu wake wa kazi bwana Andoni Zubizarreta ambaye alijiuzuru katika nafasi yake Jumatatu iliyopita.
"Kwenye taarifa yake aliyoiandika kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa facebook Puyol amesema anataka kuufahamisha umma kuwa nimekamilisha muda wangu wa kazi hapa na mahusiano yangu na klabu ya Barcelona,"
"Miezi hii mitatu na nusu niliyokaa hapa imenipa uzoefu wa kutosha sana na hivyo ni wakati muafaka kwangu kwenda kuangalia changamoto za upande wa pili alimradi kujitanua kwa namana nyingine katika masuala haya ya soka na kuandika historia mpya."
Post a Comment