KLABU ya Yanga imewafungulia mashataka waliokuwa wachezaji wake Juma
Kaseja, Emmanuel Okwi na Geilsona Santana Santos Jaja kutokana na makosa
mbalimbali ikiwemo kufanya mazungumzo na timu nyingi bila muda
unaoruhusiwa kufika.
Mwanasheria wa klabu hiyo Frank Chacha,ameiambia Goal
kuwa mbali na kuwafungulia mashtaka wachezaji hao pia imemtoza faini ya
Milioni 300 kipa Juma Kaseja kama kwa kosa la kuvunja mkataba na
milioni 26 kama fidia ya kukosa huduma yake kwa muda ambao alitakiwa
aitumikie timu hiyo.
Aidha Chacha amesema Okwi aliyekimbilia Simba anatakiwa kuilipa Yanga
dola Milioni 1 kwa kosa la kujiunga na timu nyingine huku akiwa na
mkataba wa kuitumikia timu yao na klabu ambazo zilitangaza kumwania na
ile anayoichezea hivi sasa Simba wamezishitaki FIFA ili ziweze
kuchukuliwa hatua kwa kosa la kufanya naye mazungungumzo wakati akiwa na
mkataba wa mwaka mmoja na Yanga.
Pia Mbrazili Geilson Santana Santos JAJA anatakiwa kuilipa Yanga
fidia ya dora Milion 1 za Marekeani baada ya kukatisha mkataba wake na klabu
hiyo wakati alipokwenda kwenye mapumziko mafupi na kuna taarifa hivi
sasa amepata timu nyingine. Pia mchezaji huyo atalazimika kuilipa klabu
hiyo garama za dola 3000 kwa miezi yote iliyobaki katika mkataba wake wa
sasa.
Post a Comment