Simba tayari wamewasili Mtwara tangu juzi Alhamisi
kwa ajili ya pambano hilo ambalo litakuwa la kwanza kwa kocha mpya wa
timu hiyo Goran Kopunovic.
WENYEJI Ndanda FC, bado hali si shwari pamoja na mabadili ya benchi
la ufundi yaliyofanywa na kuongezwa kwa wachezaji sita katika dirisha
dogo la usajili mwezi Desemba mwaka 2014 lakini timu hiyo imeendelea
kubaki nafasi ya 11 ikiwa na pointi 10.
Mechi ya mwisho kwa Ndanda ilikuwa Jumamosi iliyopita baada ya
kulazimishwa sare ya 1-1 na Plosi Moro na kififisha matumaini ya
mashabiki wa Mtwara kuendelea kuiona timu yao katika ligi ya msimu ujao.
Kibaya zaidi ni kwamba licha ya timu hiyo kuendelea kubaki nyumbani
uwanja wa Nangwanda Sijao lakini kesho Jumamosi watakuwa na kibarua
kigumu cha kuikabili Simba ambayo imetoka kutwaa ubingwa wa Kombe la
Mapinduzi usiku wa Jumanne kitu ambacho kinafanya mchezo huo kuwa mgumu
kwa wenyeji.
Simba tayari wamewasili Mtwara tangu juzi Alhamisi kwa ajili ya
pambano hilo ambalo litakuwa la kwanza kwa kocha mpya wa timu hiyo Goran
Kopunovic, raia wa Serbia aliyechukua nafasi ya Mazambia Patrick Phiri.
Kwa kipindi cha wiki mbili alichokuwa na kikosi cha Simba Zanzibar
ameonekana kukibadilisha na kuwa imara tofauti na kilivyokuwa mwanzoni
ambapo katika mechi nane za ligi ilizocheza imeweza kushinda mechi moja
kutoka sare sita na kufungwa mechi moja jambo ambalo Kopunovic ameahidi
kulimaliza.
Kocha wa Ndanda FC Ngawina Ngawina, katika mchezo wa kesho atakuwa
akijivunia kiungo wake Omega Seme waliyemsajili kwa mkopo kutoka Yanga
lakini amekiri timu yake bado inamapungufu hasa kwenye sehemu ya ulinzi
ambayo imekuwa ikiruhusu nyavu zake kitikishwa katika mechi mbili
walizocheza.
“Tunakutana na timu ngumu na kubwa ya Simba lakini hatuwaogopi kwa
sababu ukiangalia hata tofauti yetu kwenye ligi sisi tupo juu kwa kuwa
na pointi 10 wao wanafuata nafasi ya 12 wakiwa na pointi tisa hicho kitu
ndiyo kinatupa nguvu ya kuweza kupambana ili kupata ushindi,”amesema
Ngawina.
“Kitu kizuri kwetu nikwamba tunajua nafasi tuliyopo ni mbaya na
hatuja fanya vizuri mechi yetu iliyopita dhidi ya Polisi lakini tunataka
kuwaonyesha watu sisi ni moja ya timu bora kwa kuwafunga Simba kama
tulivyo fanya kwa Azam na kujinasua katika nafasi za mkiani,”amesema
Ngawina.
Kwaupande wake kocha wa Simba Goran Kopunovic, amesema hawajua
wapinzani wao Ndnadna FC, lakini anamatumaini na kikosi chake hakita
muangusha kama kilivyofanya kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi na
kurudi na pointi tatu Dar es Salaam.
“Nafahamu ugumu uliopo kwenye ligi ya Tanzania nimeongea na wachezaji
wanajua hali tuliyonayo na nini tunatakiwa kufanya nadhani hivyo nivitu
vya msingi kufahamu kabla hatujaingia uwanani ili kila mchezaji
akacheze kwa juhudi ili tuweze kupata ushindi lengo langu ni kubadili
matokeo ya Simba,”amesema Kopunovic.
Mserbia huyo amesema anajivunia ubora wa kikosi chake ambao umekuwa
ukiimarika siku hadi siku na hata kurejea kwa mshambuliaji Mganda
Emmanuel Okwi na Danny Sserunkuma aliyeonyesha kiwango cha juu kwenye
mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi.
“Vijana wote wapo katika hali nzuri hatuna majeruhi ukimtoa Said
Ndemla aliyeumia kwenye kombe la Mapunduzi naamini kila kitu kinakwenda
sawa na kesho kazi yetu ni moja tu katika dakika 90 kusaka pointi tatu
ambazo zinarudisha mwanga kwamashabiki wa Simba,”amesema Kopunovic.
Chanzo: Goal.com
Post a Comment