Manchester
United iko katika hatua nzuri ya kushinda mbio za kumsajili mlinzi wa
kati Aymeric Laporte mara baada ya kukubali kulipa kiasi cha paundi
milioni 32 ikiwa ni ada inayoweza kuvunja mkataba wake wa sasa na hivyo
kuwa mchezaji halali kabisa wa Man U kuanzia mwezi January.
Laporte
anayetajwa kuwa mmoja kati ya walinzi bora kabisa chipukizi kwa sasa
alikua anaviziwa sana na klabu ya Arsenal ili kuweza kuimarisha sehemu
ya ulinzi ya klabu hiyo lakini sasa imefahamika kuwa mlinzi huyo raia wa
Ufaransa rasmi atavaa jezi ya Manchester United ambapo Louis van Gaal
akijiandaa kupeleka kiasi cha paundi milioni 32 ili kumnyakua mlinzi
huyo.
Post a Comment