Wakati mambo yakionekana kana kwamba yameanza kumnyookea, kocha mpya wa klabu ya Real Sociedad, Mscotish David Moyes baada ya kupata ushindi mbele ya klabu ya Fc Barcelona sasa mambo yanaonekana kugeuka na kurejea kulekule kwenye ugumu.
Meneja huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United alitolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa timu yake ya Real Sociedad dhidi ya nyambizi wa Villarreal kwenye mchezo wa raundi ya pili ya michuano ya Copa Del Rey usiku wa jana.
Moyes hakuonekana kujali kadi hiyo kwani mara baada ya kutoka benchini na kwenda kukaa jukwaani aliamua kuanza kugonga vitafunwa vilivyokua vikiliwa na mashabiki waliokuwa wamekaa uwanjani hapo huku akionesha tabasamu zito kwa mashabiki hao.
Post a Comment