0
Arsenal star 'fined £20,000 for smoking after match'
Imearifiwa kuwa klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza imempiga faini mlinda mlango wake namba moja  Wojciech Szczesny ya paundi 20,000 mara baada ya kukutwa akivuta sigara kwenye bafu ya vyumba vya kubadirishia nguo mara baada ya mechi.

Szczesny alilaumiwa na wachezaji wenzake mara baada ya kipyenga cha mwisho cha mchezo uliomalizika kwa klabu ya Arsenal kuambulia kichapo cha jumla ya magoli 2-0 mbele ya  Southampton siku ya mwaka mpya mchezo ambao makosa aliyoyaffanya mlinda mlango huyo ndio yaliyosababisha magoli yote mawili.

Taarifa zinadai kuwa meneja wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger alikasirishwa sana na makosa aliyoyafanya mlinda mlango huyo lakini hasira zake zilizidi zaidi palealipokamatwa akivuta sigara kwenye moja ya bafu za uwanjani hapo.

Wenger ameamua kumkata kiasi hicho cha pesa ya mshahara wa mlinda mlango huyo lakini klabu ya Arsenal yenyewe mpaka sasa haijasema chochote kuhusiana na tukio hilo na walipotafutwa ili kulizungumzia suala hilo walikataa katakata kulizungumzia.

Post a Comment

 
Top