Klabu ya Arsenal inatarajiwa kuwasajili mmoja kati ya wachezaji wanne hawa kutoka nchini Ujerumani endapo kama itafikia makubaliano na vilabu au wachezaji binafsi ili kukiimarisha kikosi cahake.
Usajili wa wachezaji Per Mertesacker, Lukas Podolski na Mesut Ozil kumeleta mapinduzi makubwa sana ndani ya kikosi hicho cha The German kutokana na ubora wa wachezaji haoa hivyo endapo klabu ya Arsenal itawasajili mmoja kati ya wachezaji wafuatao ninaamini ubora wa klabu hiyo utaimarika zaidi.
1. Lars Bender
Lars ni mmoja kati ya wachezaji amabao wamekua wakiwindwa kwa muda mrefu sana na meneja wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger ikitajwa kuwa ni takribani mara mbili ofa ya klabu ya Arsenal ilitupiliwa mbali katika miaka miwili iliyopita. Huyu ni mlinzi wa kati ambaye pia ana uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa upande wa kulia atakuja kuiimarisha sana safu ya ulinzi ya klabu ya Arsenal.
2. Mats Hummels
Hummels ni mlinzi wa kiwango cha juu sana kwa sasa Duniani ambaye anaitumikia klabu yake ya sasa ya Borussia Dortmund ambayo imekua na msimu mbovu sana katika ligi kuu ya nchini Ujerumani. Klabu ya Arsenal inaweza kumnasa mlinzi huyu imara kabisa kwa ada ya paundi milioni 25 tu ili kuimarisha sehemu ya ulinzi ya klabu hiyo.
3. Sven Bender
Huyu ni kaka wa Lars Bender, Sven anakipiga kwenye klabu ya Dortmund, inayopambana isishuke daraja msimu huu kutokana na kuwa mkiani mwa msimamo wa ligi kuu ya nchini Ujerumani hivyo basi ofa nzuri itakayotolewa na klabu ya Arsenal itaweza kumshawishi mchezaji huyu kulazimisha uhamisho wake halikadhalika klabu yake ya Dortmund kujikuta ikisawishika kumuuza mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji lakini zaidi kama mlinzi wa kati kama ilivyo kwamdogo wake Lars.
4. Sami Khedira
Khedira ni mchezaji ambaye mimi mamuona kama vile tayari amekwisha tua Arsenal kutokana na ukweli kwamba kilichobakia ni mazungumzo baina yake na klabu ya Arsenal kutokana na ukweli kwamba mkataba baina yake na klabu ya Real Madrid unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu
Post a Comment