MSHINDI wa tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania kwa mwaka 2014 inayotolewa na Mtandao wa Goal.com
Mbwana Samata amewataka wachezaji chipukizi kujitambua na ili wapate
mafanikio ni lazima wajitume na waweke mbele kile ambacho wanakikusidia.
Samata aliyeshinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda wanasoka wenzake
wanne ambao ni Mrisho Ngasa, Jonas Mkude, Salum Abubakar na Thomas
Ulimwengu amesema tuzo hiyo itamuongezea ari ya kuzidi kujituma na
kufanya mazoezi kwanguvu ili aweze kushinda tena tuzo hiyo mwaka huu.
“Najisikia furaha sana kuwa mshindi wa tuzo hiyo inayotolewa kwa mara ya kwanza Tanzania na Mtandao wenu wa Goal
kwani inaonyesha ni kiasi gani mnathamini jitihada zangu na inanipa
hamasa yakuzidi kujituma na kuendelea kupokea tuzo hiyo kila mwaka kwani
inamuongezea heshima hata kwenye klabu yake anayochezea ya TP
Mazembe,”anasema .
Pia Samata aliwapongeza wachezaji aliowashinda katika mchuano huo na
kuwataka wasikate tamaa wazidi kujituma kwani licha ya kuibuka na
ushindi lakini nao walistahili kuwa washindi kutokana na kuwa na viwango
vya juu mwaka 2014, lakini anafurai kuona ameshinda yeye tuzo hiyo.
Post a Comment