Wakati usajili wa mwezi Januari ukiwa umekwishaanza kusika kasi hebu kwa pamoja tujaribu kuangalia orodha ya wachezaji wafuatao waliosajiliwa mnamo mwezi huu na kushindwa kuonesha makali yao kwenye vilabu vyao.
Sahau kuhusu akina Kim Kallstrom aliyesajiliwa kwa mkopo kwenye klabu ya Arsenal akiwa na maumivu ya mgongo wafuatao walisajiliwa wakiwa wazima bukheri wa afya lakini wakashindwa kabisa kuonesha cheche zao.
20) NICOLAS ANELKA.
Shanghai Shenhua kwenda
Juventus kwa mkopo mnamo mwaka 2013 ambapo alishindwa kabisa kuonesha cheche zake ambazo wapenzi wengi wa kandanda wamezoea kuziona.
19) MANICHE.
Atletico Madrid kwenda Inter Milan kwa mkoo mnamo mwaka 2008 mara baada ya kutokea hali ya sintofahamu baina yake na mejeja wa Atletico wa wakati huo Maniche aliamua kwenda kuomba hifadhi Inter Milan ambako alishindwa kuonesha cheche zake zilizokuwa zikitarajiwa na wapenzi wengi wa soka Ulimwenguni.
18) MARIO BALOTELLI.
Manchester City kwenda AC
Milan kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 20 mnamo mwaka 2013. Kinachostaajabisha kwa mshambuliaji huyu mtukutu ni kuwa alikuwa vizuri sana kwenye miezi sita ya mwanzo lakini alishindwa kuwapatia wana Rassoneri walichokitarajia mara baada ya kukumbwa na ukame wa mabao mapka alipooneshwa mlango wa kutokea kuelekea klabu ya Liverpool.
17) URBY EMANUELSON.
Ajax kwenda AC Milan kwa ada ya uhamisho wa paundi ilioni 2.5 mnamo mwaka 2011. Akiwa ametoka kuonesha uwezo mkubwa sana akiwa na klabu ya Ajax lakini Mbazil huyu alishindwa kuhamishia makali yake San Siro.
16) IBRAHIM AFELLAY.
PSV kwenda Barcelona mnamo mwaka 2011 kwa ada ya paundi milioni 3. Mholanzi huyu alikua katika mwaka wa mwisho kabisa wa mkataba wake na Barca ambapo Wakatalunya hao waliamua kumuonesha mlango wa kutokea pale walipoamua kumpeleka kwa mkopo kwenye klabu ya Olympiakos yanchini Ugiriki.
15) BENNI MCCARTHY.
Blackburn kwenda West Ham
United kwa ada ya paundi milioni 2.5 mnamo mwaka 2010. alisainiwa siku ya mwisho kabisa mwa dirisha la usajiri ambapo ulimshuhudia mchezaji huyu akipata majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu lakini mara baada ya kurejea aligundulika kuongezeka uzito mara dufu na hivyo mabosi wa Upton Park wakalazimika kumlipa takribani paundi milioni 1 ili kuvunja nae mkataba mwaka uliofuata.
14) THOMAS GRAVESEN.
Everton kwenda Real Madrid
kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 4 mnamo mwaka 2005. alionekana kama maji kupwa mara baada ya kushindwa kabisa kuonesha cheche zake alizozionesha kwenye michuano ya Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Norway hivyo kuishia ubaoni pale Santiago Bernabeu hivyo mara baada ya miezi sita alioneshwa mlango wa kutokea na kurejea nchini Uingereza.
13) SAMUEL KUFFOUR.
Roma kwenda Ajax kwa mkopo mnamo mwaka 2008. Awali alisaini mkataba wa mkopo wa miezi sita ikiwa kama kipindi chake cha maangalizi kabla ya kusaini mkataba wa kudumu wa miaka miwili lakini mara baada ya kukamilika kwa mkataba wake wa mkopo Ajax ilikataa katakata kumsajili mlinzi huyo na hivyo kumrudisha kwenye klabu yake ya AS Roma.
12) FABIEN BARTHEZ.
Akiwa tayari amekwishatangaza kustaafu kwake Barthez aliamua kusitisha mapumziko yake ya kudumu na kuamua kusaini mkataba na klabu ya Nantes mnamo mwaka 2007. Lakini alishindwa hata kumaliza msimu mmoja kutokana na kiwango kibovu alichokionesha hivyo aliamua kuachana na klabu hiyo na kurejea kwenye mapumziko yake.
11) MAXI LOPEZ.
River Plate kwenda FC Barcelona kwa ada ya paundi milioni 6.2 mnamo mwaka 2005. Muajentina huyu Atabakia kukumbukwa na mashabiki wengi wa klabu ya Barcelona pale alipofunga kwa mpira wake wa kwanza kuugusa alipoanza kuitumikia Barca lakini alikaa takribani miezi 18 pale Camp Nou na kuoneshwa mlango wa kutokea.
Post a Comment