0
Arsenal expect to sign Carvalho with new £21.3m transfer offer
Arsenal wanaimani ya kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho kabla ya Jumaatatu siku ambayo ndio utakua mwisho wa usajili wa majira haya ya joto kwa ada ya paundi milioni 21.3.

The Gunners wamekua wakimfuatilia Carvalho kwa takribani wiki tatu sasa na taarifa zinadai kuwa tayari Arsenal walikwisha weka ada ya paundi milioni 20 mezani ambayo ilikataliwa na mabosi wa Sporting Lisbon. 

Lakini taarifa zinadai kuwa Sporting wameamua kushusha mahitaji yao ya kumuuza mchezaji huyo na sasa Arsenal inasemekana wamerejea na ofa mpya mezani ili kumnasa kiungo huyo.

Arsenal Training Session

Imekaliliwa pia ofa ya paundi milioni £21.3 ambazo ni sawa na Euro milioni 27 ambayo Mfaransa Arsene Wenger ameiongeza itakua ni chambo ya kumnasa kiungo huyo mwenye mabavu mengi awapo uwanjani.

Post a Comment

 
Top