Arsenal na Manchester City leo wako katika nafasi nzuri ya kuuthibitishia na kuuonesha umma nini wanatarajia kwenda kukifanya kwenye mashindano mbali mbali msimu huu pale ambapo saa 12:00 kwa saa za Afrika ya mashariki watakua wanaingia kwenye mchezo wa ngao ya jamii yaani FA Community Shield.
City kwa siku za hivi karibuni wamekua wakicheza Wembley mara kwa mara kutokana na kuwa washindi wa vikombe mbali mbali vya huko mchini Uingereza.
Tofauti na Arsenal ambao watakua kwa mara ya kwanza wanakuja uwanjani hapo tangu walipocheza kwa mara ya mwiso mchezo wa Ngao ya Jamii mnamo mwaka 2005, na mara zingine walikua wakija kwaajili ya hatua mbali mbali za michuano ya FA.
Arsenal kwa msimu huu naonekana kuingia kikamirifu kwenye dirisha la usajili wakiwa na lengo la kutaka kuuondoa ukame wa misimu tisa bila ya ubingwa inaonekana ikijiamini kufanya vizuri sana kwenye mchezo huo dhidi ya Man City.
Arsenal ilimaliza ya nne kwenye msimu wa 2013/2014 ikiwa ni alama saba nyuma ya mabingwa Manchester City, lakini jambo la kukatisha tamaa zaidi kwa Arsenal kwa msimu uliomalizika ni vile ambavyo walikua wakicheza dhidi ya vilabu vikubwa kwa msimu uliokwisha huo na hivyo leo inachukuliwa ni kama siku ambayao wanatarajiwa kuuonesha na kuutangazia umma nini wanatarajia kuja kukifanya msimu huu.
Kichapo cha 6-3 pale
Etihad msimu uliopita kinaleta hisia tofauti na kuongeza ladha ya mchezo huu ingawa hii ni kumbukumbu mbaya kwa klabu na mashabiki wa Arsenal,ambao pia walicheze vichapo kutoka kwa Liverpool na Chelsea.
Arsene
Wenger anaamini kuwa klabu yake sasa iko tayali kutoa changamoto na kutwaa ubingwa msimu huu mara baada ya kuwasainisha
Alexis Sanchez, Mathieu Debuchy, Calum Chambers na David Ospina.
Wajerumani Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski ambao walikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa Dunia hawatakuwemo kwenye kikosi cha Arsenal hii leo kutokana na kupewa mapumziko mara baada ya kumaliza michuano ya kombe la dunia.
City kwa upande wao wamezileta sura kadhaa mpya katika kikosi chao wakiwemo Fernando, Willy Caballero, nao
Frank Lampard anayekipiga kwa mkopo klabuni hapo.
Bacary Sagna amenunuliwa akitokea Arsenal mara baada ya kuisha kwa mkataba wake na washika mitutu hao wa London, ambapo anakwenda kuungana na wenzake waliotokea klabuni hapo miaka kadhaa iliyopita Samir Nasri na Gael Clichy.
Meneja Manuel Pellegrini atakua bila ya Alvaro Negredo kwenye mchezo huo dhidi ya Arsenal ambye anapambana na maumivu ya mguu aliyoyapata kwenye michezo ya maandalizi ya msimu amabayo yatamuweka nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.
Mchezo huu utakua ni sehemu muafaka kwa golikipa Caballero na kiungo Fernando kuonesha uwezo wao na hatimaye kumshawishi mwalimu Mannuel Pellegrini kuwatazama kama wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Man City.
Mchezo huo utakaochezeshwa na mwamuzi Michael Oliver unatarajiwa kuwa ndio mchezo wa kwanza kutumia Spray kama zilizokua zikitumika kwenye michuano ya kombe la Dunia.
Post a Comment