Frank Lampard mwenye umri wa miaka 36 kwa sasa ametangaza rasmi kuachana na soka la kimataifa hii leo akiwa tayari amekwisha itumikia timu yake ya taifa la Uingereza kwa takaribani michezo 106 tangu alipocheza mchezo wake wa mwanzo mnamo mwaka 1999; na michuano yake ya mwisho ikiwa ni ya kombe la Dunia ya mwaka huu kule mchini Brazil.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Lampard alisema: "Nimechukua maamuzi ya kustaafu soka la kimataifa. Ni maamuzi magumu sana kwangu mimi lakini nimekua mtu wa kutafakari sana tangu nilipotoka kwenye fainali za kombe la Dunia."
"Nimekua nikikubalika sana na kuheshimika sana mbele ya mashabiki na waalimu waliokua wakinichagua kuitumikia timu yangu mara kadhaa na kila nikitazama nyuma najaribu kujenga taswira ya furaha niliyokua nikiipata kila nilipokua nivaa jezi ya timu yangu ya taifa."
Post a Comment