Tottenham wanataka kutuma ofa kwa klabu ya Manchester United Manchester United kwaajili ya mshambuliaji Javier Hernandez.
Gazeti la Mail on Sunday limeandika kuwa klabu hiyo inatarajia kutuma ofa hiyo kwa klabu ya United kabla ya kufikia mwishoni mwa wiki hii ili waweze kupata huduma za mshambuliaji Hernandez.
Hernandez anaonekana kama ni ziada kwenye kikosi cha mashetani hao wekundu wa Old Trafford na anaonekana kuvivutia vilabu kadhaa vya ligi kuu nchini Uingereza na ligi nyinginezo barani Ulaya ikiwemo klabu ya Southampton.
Lakini taarifa zinasema kuwa Mmexico huyo hatakua radhi kujiunga na klabu ndogo na atakuwa akihitaji ajiunge na moja ya vilabu vikubwa Duniani na timu pekee ambayo angalau inafikia matakwa hayo ni Tottenham..

Post a Comment