0
Eto'o undergoes medical ahead of Liverpool switch
Samuel Eto'o ameamua kuchukua maamuzi magumu kwa kuamua kuichagua klabu ya Liverpool licha ya kupokea pia ofa kabambe kutoka klabu ya Everton.

Klabu ta Everton ilijiingiza kwenye mbio za kutaka kumsainisha mshambuliaji huyo lakini kitendo cha kwenda kuwa kuwa chini ya Brendan Rodgers kinaonekana kuwa ndio sababu iliyomfanya Eto'o aichague Liverpool mbele ya Everton.

Eto'o sasa atafanyiwa vipimo vya afya nje ya Uingereza na rasmi dili la kujiunga na Liverpoo litatarajiwa kukamilika kabla ya Liverpool kuvaana na Manchester City siku ya jumatatu usiku.

Eto'o anajiunga na Liverpool akiwa mchezaji huru mara baada ya kuisha kwa mkataba wake dhidi ya matajiri wa Chelsea na tayari mapema alishakua na mazungumzo na klabu ya Ajax kabla hawajajitoa kwenye mbio za usajili wake.

Post a Comment

 
Top