Rooney akipiga free-kick kuelekea lango la Liverpool faulo ambayo iligonga ukuta na kuokolewa.
Louis van Gaal ameanza rasmi kuirejeshea heshima klabu ya
Manchester United baada ya alfajiri ya leo kuwaongoza vyema mashetani hao wekundu kutwaa kikombe cha kimataifa cha maandalizi ya msimu huko nchini Marekani kijulikanacho kama Internationa champions kikombe ambacho kilikua kikihusisha timu kutoka mataifa mbali mbaliya barani Ulaya kilicho andaliwa na kampuni ya vinywaji ya Guinness .
LvG akiufuatilia mchezo kwa ukaribu na umakini mkubwa
Phil Jones aliyakaribisha majanga kwa Manchester United bara baada ya kumuangusha Raheem Sterling mapema kabisa na mwamuzi kuwazawadia mkwaju wa penati vijogoo wa Anfield.
Lilikua ni goli la kumi kwa nahodha wa Liverpool Stephen Gerrard katika michezo inayohusisha timu hizo akiandika rekodi mpya kabisa ya upachikaji wa mabao kwa timu hizo zinapokutana.
Gerrard akipiga ukwaju wa penati uliowapa Liverpool goli la kuongoza
Rooney alifanikiwa kuisawazishia Manchester United mapema kipindi cha pili kwa goli ambalo wachambuzi wa masuala ya kisoka wanaliona kana kwamba lina utata ndani yake kwani kabla ya mfungaji kuweka mpira kimiani mpira huo ulikua tayari ushagonga mtambaa panya kwa njea na kurejea uwanjani.
Hakika mpira kweli ulitoka nje kabla ya Rooney kuukwamisha wavuni
Hatimaye mwamuzi wa mchezo aliliona kuwa ni goli halali na hivyo kufufua matumaini ya klabu ta Manchester United.Mwamuzi msaidizi alionekana kumuelekeaza mwamuzi wa kati lakini tayari wakati wachezaji wa Liverpool na mwamuzi msaidizi wakitoa maelekezo hayo mwamuzi alishakua ametoa maamuzi ya kulikubali goli hilo.
Rooney akishangilia goli la kusawazisha
Inawezekana kwa mtazamo wa harakaharaka mtu asiuone umuhimu wa mashindano na mchezo huu kwa ujulmla lakini mambo ni tofauti kwa meneja mpya wa Manchester United Van Gaal ambaye jana aliishuhudia timu yake pale mjini Miami kwenye uwanja wa Sun Life ikitoka nyuma na hatimaye kuibuka na ushindi mbele ya wapinzani wake wa jadi.
Gerrard akipongezwa na Jordan Henderson (kulia) Lambert (kushoto) baada ya kufunga
Hii inamaanisha kwamba United inarejea Nyumbani leo Jumaane asubuhi ikiwa haijafungwa hata mchezo mmoja katika ziara yao ya huko nchini marekani akiwa imecheza na moja kati ya timu bora duniani zikiwemo Real Madrid, Roma na Inter Milan.
Post a Comment