0
 
 
Al-Ahli ya nchini Misri imeweka ofa mezani kwaminajili ya kumnasa mshambuliaji wa kibrazil anayekipiga katika timu ya AC Milan Robinho.

Mmoja wa maofisa wa ngazi za juu kutoka shirikisho la soka la nchi za kiarabu UAE amethibitisha kwa kusema kuwa Al-Ahli wamekwisha kutana na wakala wa mchezaji huyo wikiendi iliyopita alikua mjini Dubai na tayari makubaliano ya awali yamekwisha fanyika na sasa maamuzi ya mwisho yamebakia kwa bodi ya Milan.



Taarifa zinasema kuwa ofa iliyotolewa na  Al-Ahli ni kubwa kuliko thamani halisi ta  Robinho na mahitaji yake binafsi tatizo linalosalia hapo ni utayari wa mchezaji mwenyewe kucheza kwenye mashindano yaliyo katika kiwango cha chini. 



 Ikumbukwe kuwa klabu inayoshiriki ligi ya MLS  ya Orlando City ya huko nchini Marekani ni miongono mwa vilabu ambavyo vinasaka saini ya mshambuliaji huyu wa kibrazil. 

Post a Comment

 
Top