West Brom imethibitisha kumnasa mshambuliaji Georgios Samaras kwa mkataba wa miaka miwili.
Samaras amejiunga na timu hiyo akiwa kama mchezaji huru anakua mchezaji wa tisa kusajiliwa na meneja wa timu hiyo Alan Irvine.
Mchezaji huyu ameiwakilisha timu yake ya taifa ya Ugiriki kwenye michuano miwili ya Dunia ametumia takribani misimu sita akiwa na mabingwa wa Scotland Celtic amesema kwa sasa anahitaji kubadilisha mazingira mara baada ya kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya West Brom zinasema klabu hiyo imefurahia kitendo cha kumpata mchezaji huyo kwani ni mmoja kati ya wachezaji wenye uzoefu mkubwa ukilinganisha na wengi walionao kwani tayari amekwisha cheza kwenye michuano ya Champions
League, European Championships hali kadhalika kombe la Dunia kitu ambacho West Brom inaamini kinampatia makali ya ziada.
Usajili wa Samaras unampa Meneja Irvine kuwa na washambuliaji wanne kutokana na usajili wao wa kuwajumuisha kikosini humo wachezaji Brown Ideye, Saido Berahino na Victor
Anichebe.
Na tayari meneja wa timu hiyo amemjumuisha kikosini mchezaji huyo kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi siku ya jumaamosi dhidi ya Southampton.
Post a Comment