0

Acceptance: Arsene Wenger is resigned to the fact Vermaelen will soon be moving elsewhere

Arsenal inaonekana kama haiko tayari kurejea tena makosa yake iliyoyafanya miaka mitatu iliyopita pale amabapo ilimwachia kiurahisi RvP kwenda Manchester United. Safari hii ikiwa Man Utd wanamsaka kwa udi na uvumba mlizi wa kati wa kibeligiji Thomas Vermaelen wakiwa na madhumuni ya kuziba pengo lililoachwa wazi na wakongwe Rio Ferdinand na Nemanja Vidic waliotimukia QPR na Inter Milan.

On his way out: Thomas Vermaelen is unwilling to enter negotiations over a new contract at Arsenal, increasing the likelihood he will leave the Emirates this summer 

Kwa mujibu wa gaazeti la London Evening Standard Arsena inaonekana kuwa tayari kukaa chini na mlinzi huyo ili kujaribu kuziondosha baadhi ya tofauti zilizojitokeza msimu uliopita.Ikimbukwe kuwa msimu uliopita Vermaelen ambaye pia ni nahodha wa Arsenal alianza kwenye michezo saba tu kwakuwa meneja wa timu hiyo Arsene Wenger aliwachagua Mjerumani na Mfaransa Per Mertesacker na Laurent Koscienlny kama walinzi wake wa kati.
 

Vermaelen amebakisha mkataba wa mwaka mmoja na washika bunduki na japo Mfaransa Arsene Wenger ameonesha nia ya kutaka kuyatatua matatizo yaliopo anaonekana kukatishwa tamaa na kitendo cha meneja wake kupoteza imani naye kwenye kikosi cha kwanza.

Vermaelen anataka kwenda United lakini Arsenal wanaonekana kutokuwa tayari kwa hilo na wangependelea kumuona Tom akienda kucheza nje ya EPL kwani Arsenal bado inabakia na kumbu kumbu kwamba kufanya hivyo itakua ni mara ya pili kwa nahodha wa timu hiyo kutimkia Old Traford ndani ya miaka mitat.


Ukiachilia mbali Manchester United pia Vermaelen anasakwa pia na vilabu vya Barcelona ambao wameshatangaza kuweka mezadi dau la Euro milioni 15 (paundi milion 10) hali kadhalika klabu ya napoli nayo imeingia kwenye mbio za kuisaka saini ya Mbeligiji huyo.

Post a Comment

 
Top