kiungo wa Cardiff Jordon Mutch anakaribia kukamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Queens Park Rangers iliyopanda daraja msimu huu mara baada ya kuteremka msimu uliopita.
Klabu hiyo ya Wales imekubali ofa inayokadiliwa kufikia paundi milion 6 kwaajili ya kukamilisha dili la kiungo huyo.
Mutch,aliyeifungia cardif jumla ya magoli saba kwenye Premier League msimu uliopita anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na kutambulishwa rasmi pale Loftus Road leo jumaane.
Anakwenda kuwa mchezaji wa pili kununuliwa na QPR kutoka Cardiff, baada ya uhamisho wa paundi milioni 8 mtangulizi wake Steven Caulker.
Tineja huyo mwenye miaka 22 alianza kuitumikia Birmingham City, kabla ya kwenda jijini London kwa mkopo kuitumikia Watford kwenye msimu wa mwaka 2010-11
msimu ambao alifunga takribani magoli matano katika michezo 23 alitoichezea timu hiyo.
pia zipo taarifa zinazomuhusu kiungo wa Chile aliyekipiga kwenye World Cup Gary Medel ambaye anajiandaa kuondoka ndani ya klabu ya Cardiff, kwa ada inayosemekana kufikia kiasi cha paundi milioni 10 tayari kabisa kujiunga na mabingwa wa zamani wa Serie A Inter
Milan.
Timu hizo tayari zimeshafikia makubaliano yote na sasa kinachosubiriwa ni malipo tu ili kila mtu aweze kufa na chake.
Post a Comment